Sale!
Sale!
Sungura na Mbwa 4a (EAEP) Sungura na Mbwa 4a (EAEP)
Original price was: KSh233.00.KSh210.00Current price is: KSh210.00.
Category
KSh233.00 Original price was: KSh233.00.KSh210.00Current price is: KSh210.00.
Tuliondoka pale maziarani, mama akiwa mbele yetu kuongoza rubaa hadi kiamboni.Nilimtazama alivyotembea. Alikuwa mnyonge, gofu la mtu, kabaki mitulinga ,nyonga na fuvu la kichwa. Alikuwa mnyonge mfano wa sabatele changaraweni. Tulitembea guu bandika guu bandua. Kimya. Unywele ungalianguka, ungaliusika
Siku hii naikumbuka kama jina langu…..
ISBN : 9789966342355
Katika nchi ya Tofali, paliondokea mti ambao ulishangaza kila mtu. Alfajiri, majani ya mti huo yaligeuka rangi na kuwa ya buluu, mchana yakawa ya kijani, alasiri yakawa njano, jioni yakawa ya hudhurungi na meusi usiku. Jinsi mti huo ulivyokua kwa kimo, ndivyo ulivyopanuka. Mti huo ulitisha. Hakuna mtu aliyethubutu kuukaribia.Siku moja vijana wawili wakakamavu waliamua kuukaribia. Je, waliangamizwa na mti huo wa ajabu au walirudi kijijini wakiwa wazima?
ISBN: 9789966342508
Juma na Maria ni wanafunzi wa darasa la kwanza. Wao hufanya mambo mbalimbali kila siku. Mambo ambayo wanafanya nyumbani ni tofauti na mambo wanayofanya shuleni. Soma kitabu hiki. Utajua ni mambo gani Juma na Maria wanafanya.
ISBN: 9789966342478
Sudi ni mvulana aliye na sifa za kiajabuajabu tangu anapozaliwa. Anazaliwa usiku wa manane, anatabasamu na ana sura jamali. Anapoanza kukua, anawashangaza wazazi na ndugu zake kwa jinsi anavyoelewa na kufanya mambo kwa haraka tofauti na watoto wengine. Vitendo vya Sudi pia vinawashangaza wanakijiji. Mambo mengi anayoyafanya Sudi yanawafanya watu kuamini kuwa yeye si mvulana wa kawaida. JE, Ni mambo yapi anayoyafanya Sudi na yanayowashangaza wengi?
ISBN : 9789966342690
Kito, msichana mdogo wa shule ya msingi, ana kipawa cha kuimba. Kila apatapo nafasi anakuza kipawa hicho. Mwalimu anapomtafuta mwanafunzi ambaye atamtumbuiza mgeni mkuu, wanafunzi wanamchagua Kito.Je, ataweza jukumu hilo? Kito Apepeta kimeandikwa kwa ustadi mkubwa. Kitabu hiki kinawalenga watoto wanaoanza kukamaa kwa lugha no fasihi. Kinaburudisha na kuwahimiza watoto kukuza vipaji vyao.
ISBN: 9789966788174
Reviews
There are no reviews yet.