Sale!
Sale!
Sungura na Mbwa 4a (EAEP) Sungura na Mbwa 4a (EAEP)
Original price was: KSh233.00.KSh210.00Current price is: KSh210.00.
Category
KSh233.00 Original price was: KSh233.00.KSh210.00Current price is: KSh210.00.
Huu ni mkusanyiko wa hadithi kumi na mbili, zenye mafunzo sufufu katika jamii ya leo. Ni hadithi ambazo zitakufanya uache kula pilau kwa samaki ili uzisome kwanza! utakapokuwa ukizisoma, zitakufanya usahau ulikuwa na mlo mezani kutokana na ucheshi uliomo. Hadithi hizi zinanuia kuwafundisha wanafunzi maadili ili wajenge mustakabali.
ISBN: 9789966140029
Roda ni msichana mdogo ambaye ana ndoto ya kufanikiwa maishani – ndoto ya kuwa jaji. Maisha katika kijiji cha Tupe si rahisi hata kidogo. Kwanza anatoweka asijulikane alipo. Pili mama yake anauawa kinyama na watu wasiojulikana. Baada ya mazishi ya mama yake, mjomba wake Bwana Kilemba anamchukua ili kumtunza. Mke wake Bibi Mnuna yuaonekana kutopendezwa na hatua hiyo. Anageuka kuwa katili kwake Roda. Je, Roda ataweza kuitimiza ndoto yake mikononi mwa Mnuna? Usisubiri kuambiwa uisome hadithi hii.
ISBN: 9789966075628
Ziara ya Meno Siku ya Meno ni hadithi ya pili katika msururu wa “Mazingira na Afya’.
Kitabu hiki kinashughulikia usafi na afya ya meno. Lengo hili limetimizwa kupitia safari ya akina Baraka na Zawadi.
Njia za kutunza meno na athari za kutoyatunza zimewekwa wazi kupitia majadiliano baina ya wahusika.
Je, wahusika wananufaika mwisho wa kikao?
ISBN: 9789966788849
Kito, msichana mdogo wa shule ya msingi, ana kipawa cha kuimba. Kila apatapo nafasi anakuza kipawa hicho. Mwalimu anapomtafuta mwanafunzi ambaye atamtumbuiza mgeni mkuu, wanafunzi wanamchagua Kito.Je, ataweza jukumu hilo? Kito Apepeta kimeandikwa kwa ustadi mkubwa. Kitabu hiki kinawalenga watoto wanaoanza kukamaa kwa lugha no fasihi. Kinaburudisha na kuwahimiza watoto kukuza vipaji vyao.
ISBN: 9789966788174
Ni wakati wa usiku, usiku wa mashetani wakati kijana Fadhili anapozinduka na kumfumania baba yake akiufunga mlango wa chumba chake. Ni baba anayetekeleza mpango wa siri asiofaa kuujua Fadhili.
Fadhili anaamua kukitegua kitendawili cha tukio hilo kwa kujiingiza katika hatari zisizo kifani. Hii ni mojawapo ya hadithi ambayo imefumwa ikafumika mfumo ambao utamshangaza yeyote atakayeisoma.
ISBN: 9789966075604
Reviews
There are no reviews yet.