Sale!
Sale!
ATIENO SKIPS TO THE CITY EAEP
Original price was: KSh300.00.KSh230.00Current price is: KSh230.00.
Category
KSh300.00 Original price was: KSh300.00.KSh230.00Current price is: KSh230.00.
Kito, msichana mdogo wa shule ya msingi, ana kipawa cha kuimba. Kila apatapo nafasi anakuza kipawa hicho. Mwalimu anapomtafuta mwanafunzi ambaye atamtumbuiza mgeni mkuu, wanafunzi wanamchagua Kito.Je, ataweza jukumu hilo? Kito Apepeta kimeandikwa kwa ustadi mkubwa. Kitabu hiki kinawalenga watoto wanaoanza kukamaa kwa lugha no fasihi. Kinaburudisha na kuwahimiza watoto kukuza vipaji vyao.
ISBN: 9789966788174
Sudi ni mvulana aliye na sifa za kiajabuajabu tangu anapozaliwa. Anazaliwa usiku wa manane, anatabasamu na ana sura jamali. Anapoanza kukua, anawashangaza wazazi na ndugu zake kwa jinsi anavyoelewa na kufanya mambo kwa haraka tofauti na watoto wengine. Vitendo vya Sudi pia vinawashangaza wanakijiji. Mambo mengi anayoyafanya Sudi yanawafanya watu kuamini kuwa yeye si mvulana wa kawaida. JE, Ni mambo yapi anayoyafanya Sudi na yanayowashangaza wengi?
ISBN : 9789966342690
Ni wakati wa usiku, usiku wa mashetani wakati kijana Fadhili anapozinduka na kumfumania baba yake akiufunga mlango wa chumba chake. Ni baba anayetekeleza mpango wa siri asiofaa kuujua Fadhili.
Fadhili anaamua kukitegua kitendawili cha tukio hilo kwa kujiingiza katika hatari zisizo kifani. Hii ni mojawapo ya hadithi ambayo imefumwa ikafumika mfumo ambao utamshangaza yeyote atakayeisoma.
ISBN: 9789966075604
Dafina ya Ushairini diwani yenye kutoa mwanga katika
fani ya ushairi kwa shule za msingi. Huu ni mkusanyiko wa mashairi
mepesi ambayo yametungwa kufundi kwa kuangazia maudhui mapana tangia nidhamu,
maadil, bidii, elimu, mazingira na masuala mengine ibuka.
ISBN: 9789966140180
Ali ni mwanafunzi wa Darasa la Kwanza. Mahali anakoishi kuna vitu vya aina nyingi. Vitu hivyo vina rangi mbalimbali. Ali anazipenda rangi hizo. Ungana na Ali katika kitabu hiki. Utajua vitu na rangi zake.
ISBN: 9789966342676
Reviews
There are no reviews yet.