KSh350Original price was: KSh350.KSh250Current price is: KSh250.
The NPPE Reading Scheme forms an important part of the New Progressive Primary English (NPPE) course. The storybooks for each grade are specially written to emphasize specific language skills learnt in the main course. Here is a reading scheme that offers the modern child an excellent mix of graded stories all packed with many exciting…
KSh278Original price was: KSh278.KSh250Current price is: KSh250.
The NPPE Reading Scheme forms an important part of the New Progressive Primary English (NPPE) course. There are storybooks for each class specially written to emphasize specific language skills learnt in the main course. Here is a reading scheme that offers the modern child an excellent mix of graded stories all packed with many exciting things. Now the child has fun that’s built to last. Malaika is going home from school. She starts playing around an anthill. Then some very strange things happen to her.
KSh480Original price was: KSh480.KSh350Current price is: KSh350.
Ainea anaitalii sayari yenye vimbwanga vya kila nui kwa madhumuni ya kupata haki. Safari yake inakumbwa na vikwazo na visiki aina ainati vinavyokaribia kumkatisha tamaa. Pamoja na umri wake mdogo, usuli wake uliogubikwa na ukungu mzito unamfanya kuwa windo rahisi kwa makucha ya walimwengu. Hali yake inadorora zaidi kwa kufikwa na ukiwa wa kuachwa na…
KSh355Original price was: KSh355.KSh320Current price is: KSh320.
Natija na faraja vyote hutoka mbali. Nikipiga darubini nyuma ninaona jinsi maisha yalivyonidunga miiba mikali kila sehemu ya mwili wangu. Zipo siku nilikuwa ninatumia mbalamwezi kutalii vitabu vyangu usiku baada ya kukosa mafuta taa. Mwangaza hafifu nilioutumia pamoja na moshi uliotoka kwenye koroboi nilipokuwa nikisoma usiku, viliyaharibu macho yangu hadi leo ninavaa miwani…
KSh228Original price was: KSh228.KSh205Current price is: KSh205.
Katika nchi ya Tofali, paliondokea mti ambao ulishangaza kila mtu. Alfajiri, majani ya mti huo yaligeuka rangi na kuwa ya buluu, mchana yakawa ya kijani, alasiri yakawa njano, jioni yakawa ya hudhurungi na meusi usiku. Jinsi mti huo ulivyokua kwa kimo, ndivyo ulivyopanuka. Mti huo ulitisha. Hakuna mtu aliyethubutu kuukaribia.Siku moja vijana wawili wakakamavu waliamua kuukaribia. Je, waliangamizwa na mti huo wa ajabu au walirudi kijijini wakiwa wazima?
KSh422Original price was: KSh422.KSh380Current price is: KSh380.
SOMA PAMOJA NA MTOTO WAKO Furahia uhondo wa kusoma pamoja na mtoto wako.
Mtoto wako atavipenda vitabu maishani mwake na atajifundisha kwa wepesi endapo
utazingatia hoja kumi rahisi zilizoorodheshwa hapa chini.
1. Soma pamoja na mtoto wako katika mazingira yaliyotulia kama vile kwenye
chumba cha kulala.
2. Mhimize mtoto awe na mazoea ya kusoma hadithi nzima kwa kutumia
viziada vya lugha kama vile kupandisha sauti. Asome hadithi nzima kwanza
akilenga kuifurahia tu kisha aisome tena ili ajue yaliyomo.
3. Mhimize mtoto ayaashirie maneno kwa vidole hasa anaposoma hadithi
aliyokwisha kuisoma awali.
4. Chunguza kama mtoto anaelewa aliyoyasoma kwa kumuuliza maswali rahisi
kuhusu michoro, wahusika na hadithi kwa jumla.
5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu hatua anayopiga mtoto katika usomaji
wake. Usimvunje moyo bali umsifu kwa kila hatua anayopiga.
6. Hakikisha kwamba mtoto anaisoma hadithi mara kadhaa.
7. Baada ya mtoto kuzoea kusoma hadithi fulani, mhimize ajaribu kukusomea
baadhi ya maneno ya hadithi hiyo au hadithi nzima,
8. Mnunulie mtoto wako vitabu tofauti tofauti vya kuburudisha kama vile vitabu
vya picha, vya kuchekesha na vya kuelimisha.
9. Mwonyeshe mtoto wako kwamba una nia ya kufuatilia na kujua hadithi
anazozisoma kwa kumuuliza maswali kuhusu hadithi hizo. Pia mhadithie
hadithi ulizosoma kwenye vitabu ulivyo navyo.
10.Uwe kielelezo bora kwa mtoto wako ili avithamini vitabu. Mwache mtoto
wako akuone wewe ukisoma vitabu vingi.