Urafiki wa Siafu na Ndege
Original price was: KSh444.00.KSh400.00Current price is: KSh400.00.
Siafu anaenda mtoni kunywa maji. Akiwa kando ya mto anateleza na kuingia majini. Je, Ndege aliyekaribu anamwokoa? Akimwokoa, atamsaidia Ndege vipi?
Category
KSh444.00 Original price was: KSh444.00.KSh400.00Current price is: KSh400.00.
Siafu anaenda mtoni kunywa maji. Akiwa kando ya mto anateleza na kuingia majini. Je, Ndege aliyekaribu anamwokoa? Akimwokoa, atamsaidia Ndege vipi?
Roda ni msichana mdogo ambaye ana ndoto ya kufanikiwa maishani – ndoto ya kuwa jaji. Maisha katika kijiji cha Tupe si rahisi hata kidogo. Kwanza anatoweka asijulikane alipo. Pili mama yake anauawa kinyama na watu wasiojulikana. Baada ya mazishi ya mama yake, mjomba wake Bwana Kilemba anamchukua ili kumtunza. Mke wake Bibi Mnuna yuaonekana kutopendezwa na hatua hiyo. Anageuka kuwa katili kwake Roda. Je, Roda ataweza kuitimiza ndoto yake mikononi mwa Mnuna? Usisubiri kuambiwa uisome hadithi hii.
ISBN: 9789966075628
Kulanga alizaliwa katika maingira magumu yasiyosikika wala kutajika.
Hali hii haikulua ndoto yake ya kufanikiwa Tabia njema na bidii yake
zilimfanya aheshimike na walimu pamoja na wenzake shuleni
Wavyele wake walipoipa dunia kisogo, ilionekana kana kwamba hataweza kufikia ile ndoto ya ajabu aliyokuwa nayo.
Mfadhili wake anauawa kwa sumu na kisha mke wa mfadhili kukatisha ufadhille kijana huyu atafanyaje i kufanikiwa
maishani na kuifikia ndoto yake?
ISBN: 9789966075260
Katika nchi ya Tofali, paliondokea mti ambao ulishangaza kila mtu. Alfajiri, majani ya mti huo yaligeuka rangi na kuwa ya buluu, mchana yakawa ya kijani, alasiri yakawa njano, jioni yakawa ya hudhurungi na meusi usiku. Jinsi mti huo ulivyokua kwa kimo, ndivyo ulivyopanuka. Mti huo ulitisha. Hakuna mtu aliyethubutu kuukaribia.Siku moja vijana wawili wakakamavu waliamua kuukaribia. Je, waliangamizwa na mti huo wa ajabu au walirudi kijijini wakiwa wazima?
ISBN: 9789966342508
Kito, msichana mdogo wa shule ya msingi, ana kipawa cha kuimba. Kila apatapo nafasi anakuza kipawa hicho. Mwalimu anapomtafuta mwanafunzi ambaye atamtumbuiza mgeni mkuu, wanafunzi wanamchagua Kito.Je, ataweza jukumu hilo? Kito Apepeta kimeandikwa kwa ustadi mkubwa. Kitabu hiki kinawalenga watoto wanaoanza kukamaa kwa lugha no fasihi. Kinaburudisha na kuwahimiza watoto kukuza vipaji vyao.
ISBN: 9789966788174
Ziara ya Meno Siku ya Meno ni hadithi ya pili katika msururu wa “Mazingira na Afya’.
Kitabu hiki kinashughulikia usafi na afya ya meno. Lengo hili limetimizwa kupitia safari ya akina Baraka na Zawadi.
Njia za kutunza meno na athari za kutoyatunza zimewekwa wazi kupitia majadiliano baina ya wahusika.
Je, wahusika wananufaika mwisho wa kikao?
ISBN: 9789966788849
Reviews
There are no reviews yet.